29 Aprili 2025 - 19:54
Source: Parstoday
Shirika la Haki za Binadamu la Euro-Med: 94% ya waliouliwa na mashambulio ya Israel Ghaza ni raia

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Ulaya na Mediterania, Euro-Med Human Rights Monitor limeyatoa maanani madai ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba majeshi yake yanapambana na wapiganaji wa Hamas huko Ghaza likisititiza kuwa kwa uchache asilimia 94 ya waathirika wa mashambulio ya kinyama ya utawala huo ni raia.

Euro-Med imesema, majeshi ya utawala ghasibu wa Israel yamewaua Wapalestina 345 na kuwajeruhi wengine 770 ndani ya kipindi cha siku saba tu kuanzia Aprili 20 hadi 26.

Kwa mujibu wa Euro-Med, zaidi ya nusu ya Wapalestina waliouawa shahidi katika kipindi hicho cha wiki moja walikuwa watoto, asilimia 16 kati yao walikuwa wanawake, na asilimia 8 walikuwa ni wazee.

Taarifa ya shirika hilo la kutetea haki za binadamu imeendelea kubainisha kuwa, hata akthari ya wanaume watu wazima waliouawa katika mashambulizi ya jeshi la Israel walikuwa wakifanya kazi za kiraia au za taaluma huru zisizohusiana na harakati zozote za kijeshi au za kimashirika.

Euro-Med imesisitiza kuwa, sambamba na ongezeko kubwa la vifo na maafa ya raia wa Ghaza, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anakanusha hadharani kuwa jeshi la Kizayuni linawalenga raia.

Limeuelezea uwongo unaosemwa na Netanyahu kuwa ni jaribio la wazi la kupotosha na kujaribu kuhadaa maoni ya umma kimataifa na kuficha uhalifu unaofanywa katika mazingira halisi ya Ukanda wa Ghaza.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limesisitiza kuwa kuongezeka idadi ya maafa ya vifo na majeruhi wanayopata raia wa Ghaza kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa kunasadifiana na kuendelea kutolewa na Netanyahu taarifa za uongo kupitia vyombo vya habari, za kukanusha hadharani kuwa jeshi la Kizayuni linawalenga raia.

Halidhalika, Euro-Med imelaani kimya kinachoonyeshwa kimataifa kuhusiana na mauaji ya halaiki yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina, na kuitaja hali hiyo kuwa ni kufeli kimaadili na ni ukiukaji mkubwa wa utekelezaji wa wajibu wa kisheria kwa mataifa na jamii ya kimataifa.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza, Wapalestina wasiopungua 52,314 wameuawa shahidi hadi sasa na wengine 117,792 wamejeruhiwa tangu Oktoba 7, 2023 kutokana na vita vya kinyama na mauaji ya kimbari yaliyoanzishwa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya eneo hilo lililowekewa mzingiro.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha